Kuelewa-rehema-ya-mwenyezi-mungu
Kuelewa-rehema-ya-mwenyezi-mungu
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2013
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Kuelewa-rehema-ya-mwenyezi-mungu
Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni mfululizo wa makala zilizoandikwa na mwanachuoni mahiri Dkt. Mohammad Ali Shomali wa Iran. Katika makala hizi mwandishi anazungumzia kuhusu Rehema ya Allah (s) kwa viumbe Wake Rehema ni neema kubwa ambayo Allah amewaruzuku viumbe Wake wote. Hata hivyo, Allah ameigawa rehema hii katika sehemu mbili; kwanza hapa ulimwenguni kwa viumbe wote bila kujali kama wao ni waumini au la, na sehemu ya pili itakuwa ni Akhera kwa ajili ya watu wema tu. (Allah atujaaliye tuwe miongoni mwa watu wema Amin.)
Mwandishi ameelezea kwa kina kuhusu rehema na maana yake, na kwa kufanya hivyo amenukuu aya nyingi za Qur’ani Tukufu na Hadithi. Kwa mfano mwandishi amenukuu hadithi moja kutoka kwa Imam Baqir AS aliposema kwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Musa: ”Ewe Musa! Nipende Mimi na uwafanye Watu wangu wanipende Mimi.” Musa akasema: “Mola wangu. Unajua kwamba hapana mwingine ninayempenda mimi kuliko Wewe. Hata hivyo, [niambie] nitawezaje kuwafanya watu wengine wahamasike kukupenda Wewe zaidi?” Allah akamuambia: “Wakumbushe waja Wangu kuhusu neema na baraka Zangu kwao.”