Kuhuzunika n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

Kuhuzunika  n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

Kuhuzunika n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

Number of volumes :

1000

Publish number :

Toleo la kwanza

Publish location :

Dar es Salaam, Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Kuhuzunika n na K Kuomboleza Harakati za Bibi Zainab

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni kazi nyingine nzuri ya Ustadh Seyyid Jawad Naqavi. Tukio la Karbala na Ashura ambalo ni bahari yenye lulu zake zilizowekwa ndani kwenye kina, zinaweza tu kugunduli-wa na wale ambao wamelainishwa kabisa kwa fikra za Imamu Khomein (r.a) na kufanya mapinduzi ya marekebisho ya moyo wa kijamii katika jamii ambayo imeathiriwa na maradhi ya kijamii na ya vikundi mbali mbali vya kijamii. Huu ulikuwa ujumbe wa Imamu Husein (a.s), njia ya Kiongozi wa Mashahidi (wahanga) na hali halisi ya safari ya mateka kutoka Karbala kwenda mji wa Kufa, na kutoka Kufa mpaka Syria. Safari hii ya shujaa dada yake Husein Ibn Ali (a.s) aliibadilisha kuwa harakati ambayo ilionekana kama iliyolengwa kubadilishwa kuwa kama safari ya mateka masikini, wanyonge na wachovu. Hutuba za Bibi Zainab (as) zilizopakwa rangi ya damu ya Husein na masahaba zake watukufu iliutikisa umma na ufalme wa Yazid. Ilikuwa ni juhudi za watoto wa Fatima na Ali (as) – Husein na Zainab (as) - ambazo zimeifanya Karbala kuwa Hamasa ya kudumu na kuvunja majaribio yote katika zama tofauti ya kubadilisha tukio hili kuwa ugomvi wa kifamilia au tukio linalofaa tu kufanyiwa kum-bukumbu, kupatisha thawabu na kafara la dhambi. Kitabu hiki ni tarjuma ya makala tatu zilizoandikwa na Ustadh Syed Jawad Naqvi katika jarida lake linalotoka kila baada ya miezi miwili; bi-monthly magazine Mashrabe Naabla mwezi wa Muharram – Safar. Vilevile kitabu hiki kina sura ya mwisho ambayo ni moja ya tarjuma ya hutuba nyingine. Sura zote nne katika kitabu hiki zimelenga katika kumuamsha msomaji na kufanya maumivu katika moyo wake kuelekea kwenye mateso katika zama yake ambayo ni kioo cha taswira ya kile ambacho kilitokea wakati wa Imamu Husein (a.s). Chini ya mwanga wa hatua za Imam Husein, maneno na tabia yake, kitabu hiki humshawishi msomaji kwamba wakati hali inayokuzunguka ni sawa na ilivyokuwa wakati wa Husein Ibn Ali (as) na Zainab bint Ali (as), basi na wewe vilevile unahitaji kuonesha tabia kama ile ile iliyooneshwa na watu wa Karbala. Hakuna uhalali au sababu yoyote ambayo itakubaliwa kwa ajili ya kukaa kimya bila kufanya chochote wakati watawala madhalimu wanatawala jamii, wakati maziwa na mito ya maji inapobadilika kwa damu za watu wasio na hatia. Sura ya kwanza ya kitabu hiki ambayo ni mada ya kitabu hiki huelezea na kufichua asili halisi ya Azadari ambayo ni harakati ya haki kuelekea kwenye kuiangamiza dhulma na ukandamizaji. Katika sura ya pili, ambayo imepewa jina la “Ujumbe wa Ashura” ambao kama haukueleweka unakuwa chanzo cha msingi cha kudorora na ukosefu wa harakati. Sura ya tatu juu ya “Hamasa-e-Husein” huwasilisha jina halisi la somo la tukio la Karbala ambalo limekuwa lenye kuathiriwa na upotofu na limegeuka kuwa kitu kingine mbali na kitu kinachohusika na harakati. Sura ya nne ina habari kama zile zile za sura ya tatu lakini pamoja na uchambuzi wa kihis-toria na mazingira ambayo yaliwafanya watu wapoteze matumaini na kuwa chini ya shinikizo lenye matokeo ya ukimya. Kitabu hiki ni johari nyingine na ni kazi ambayo haiishii kwa Mashia tu, bali ni kitabu cha Ummawote wa Kiislamu, na kwa kweli kwa wale wanadamu wote ambao wana maadili fulani yaliyo hai ndani yao. Namshukuru sana Allah (s.w.t) mara nyingine tena kwa kunibariki kwa fursa hii kubwa kuwa njia ya kufikisha ujumbe huu wa haki, wenye kuamsha harakati kwa jumuiya ya wazungumzaji wa Kiingereza (na sasa kwenye jumuiya ya wazungumzaji wa Kiswahili). “Ewe Allah! Wakati wowote kama kuna haja ya huduma kwenye dini Yako, nipe kipaumbele na nifanye mimi wa mbele zaidi kama njia ya kufikisha.” Imam Sajjad (a.s).