malezi ya watoto katika uislamu
malezi ya watoto katika uislamu
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
malezi ya watoto katika uislamu
Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake kimeandikwa kwa Kiingereza na jopo la maulamaa wa Misri kwa jina la Child Care in Islam. Sisi tumekiita: Malezi ya Watoto katika Uislamu. Kama inavyofahamika kwamba; Uislamu ni dini na ni mfumo wa maisha, basi mafundisho yake hayakuacha kitu kinachohusiana na maisha ya mwanadamu - kuanzia tumboni mwa mama yake, kuzaliwa kwake, kunyonya na kulikizwa kwake, kufunzwa mambo ya kimsingi na mama yake, mpaka kufikia kimo cha kwenda shuleni. Haya yameelezwa kwa utaratibu mzuri sana kutoka kwenye vyanzo viwili vikubwa vya sheria ya Kiislamu - Qur'ani na Sunna. Kwa mujibu wa Uislamu kipindi cha mafunzo ya watoto huanza wakati mwanaume na mwanamke wanapoingia katika ushirika wa ndoa, kama wazazi wa baadaye, ni lazima wajihisi kwamba wana wajibu wa kuwalea watoto wao. Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa kanuni za kurithi (tabia), mwenendo wote wa tabia nzuri na mbaya wa wazazi hurithiwa na watoto wa wazazi hao. Hivyo, mzazi akiwa na tabia nzuri atawarithisha watoto wake tabia hiyo, na ni kwa sababu hii mafunzo ya watoto huanzia punde tu wakati mume na mke wanapoingia katika ndoa. Ili kufanikisha somo la kitabu hiki, jopo hilo la maulamaa limerejea sana kwenye vyanzo hivyo viwili - Qur'ani na Sunna. Watoto ni taifa la kesho, na ili kuwa na taifa zuri lenye maadili mema, lazima kuwalea watoto katika mazingira mazuri ya kimaadili; na ni mafunzo ya Kiislamu tu, kama yatafundishwa vizuri na kuzingatiwa basi Umma utaondokana na matatizo mengi ya kijamii kama inavyoonekana hivi sasa. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan katika wakati huu ambapo jamii inazidi kudidimia katika maovu kutokana na kumomonyoka kwa maadili mema. Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu A. Mohamed kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha uchapishaji kitabu hiki.