Malumbano baina ya Sunni na Shia
Malumbano baina ya Sunni na Shia
Author :
Publisher :
Publication year :
2004
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
Malumbano baina ya Sunni na Shia
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni kitabu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na Sheikh Abdilahi Nassir kwa jina la “Malumbano Baina ya Sunni na Shia”, Kitabu hiki, “Malumbano Baina ya Sunni na Shia “ ni matokea ya khutba zake nyingi zenye kuelimisha, nyingi zikuwa kwenye kanda za kaseti na CD, mihadhara, darasa zake na tafakari ya muda mrefu. Malumbano sio ugomvi (wanavyoweza kutafsiri watu wengine) bali ni kuulizana maswali na kujibizana kwa njia ya kistaarabu, hoja, elimu na akili. Na hivi ndivyo alivyofanya Sheikh wetu huyu kwa kuandika kitabu hiki kwa mtindo wa maswali na majibu, ili kumfanya msomaji aelewe upande ule una maswali gani na upande huu una majibu gani kuhusu maswali hayo. Na kama alivyoeleza Sheikh katika utangulizi wake kwamba njia hii huenda ikamsaidia Shia anapokabiliwa na maswali kama haya, bali pia itamsaidia Sunni kuelewa sababu za Mashia kuamini wanayoamini. Na sisi tuko pamoja na Sheikh katika hili.