Mariam-Yesu-na-Ukristo-kwa-mtazamo-wa-kiislam

Mariam-Yesu-na-Ukristo-kwa-mtazamo-wa-kiislam

Mariam-Yesu-na-Ukristo-kwa-mtazamo-wa-kiislam

Publication year :

2008

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mariam-Yesu-na-Ukristo-kwa-mtazamo-wa-kiislam

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingerezakwa jina la, Mary, Jesus and Christianity: An Islamic Perspective. Sisi tumekiita, Mariamu, Yesu na Ukristo: Kwa Mtazamo wa Kiislamu.
Kitabu hiki ni matokea ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni wa Kiislamu aitwaye Mohammad Ali Shomali Waislamu wanaamini kwamba idadi ya Mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu ni zaidi ya 124,000 - wa kwanza wao ni Adam (a.s.) na wa mwisho wao ni Muhammad (s.a.w.). Miongoni mwa Mitume hao, wako
ambao Mwenyezi Mungu amewatukuza zaidi kuliko wengine, akiwemo Isa (Yesu) bin Maryam (Mariamu): “Mitume hao tumewafadhilisha baadhi yao zaidi kuliko wengine. Miongoni mwao yuko ambaye Mwenyezi Mungu alisema naye; na wengine akawapandisha vyeo, na tukampa Isa mwana wa Maryam dalili zilizo wazi na tukamtia nguvu kwa roho takatifu...” (Qur’ani 2:253)
Ingawa Mitume wote kazi yao ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa wanadamu, lakini wao ni kama walimu ambao kazi yao ni kufundisha, isipokuwa tu hutofautiana katika ufundishaji, k.v. wako wanaofundisha shule za msingi ambao hawalingani na wanaofundisha shule za sekondari na ambao hawalingani na wanaofundisha katika vyuo vikuu. Lakini pamoja na kutolingana huko, wote kazi yao ni kufundisha - ni walimu: “Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na wenye kuamini, wote wamemwamini Mwenyeezi Mungu, na Malaika Wake, na
Vitabu Vyake, na Mitume Yake, (husema): ‘Hatutofautishi baina ya Mitume Wake’ ...” (Qur’an 2: 285). Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, kwani kitawaleta karibu na kujuana wafuasi wa dini hizi mbili - Uislamu na Ukristo. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa
lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na kijamii.
Tunamshukuru ndugu yetu, Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.