Masala-ya-Kifiqhi
Masala-ya-Kifiqhi
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2010
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Masala-ya-Kifiqhi
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Masaa'ilu 'l-Fiqhiyyah , kilichoandikwa na mwanachuoni mashuhuri wa Kiislamu, Marehemu Sayyid Abdulhusain Sharafuddin al-Musawi. Sisi tumekiita, Masiala ya Kifikihi. Kitabu hiki huelezea hitilafu zilizopo baina ya Shia na Sunni kuhusu masiala (mas'ala) ya kifikihi na matendo mengine ya kiibada. Wafuasi wa madhehebu hizi wamekuwa wakishutumiana na kila upande ukiona upande wa mwenzake kuwa umepotoka. Sheria zote za Kislamu ziwe za matendo ya kiibada au za kimaisha chimbuko lake ni kutoka kwenye Qur'ani na Sunna, na madhehebu zote za Kiislamu zinakubaliana na kaida hii.
Hivyo, mwanachuoni huyu mkubwa wa Kiislamu anajaribu kuyachambua masiala haya ya kifikihi (kifqhi) ambayo madhehebu hizi hutofautiana kwa kutoa dalili na hoja kutoka kwenye Qur'ani na Sunna na pia matukio ya kihistoria kwa kutumia hoja za kielimu na ujuzi alionao. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.
Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu, Shafi Mohamed Nina kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.