Maswali-na-mishkili-elfu-sehemu-ya-kwanza

Maswali-na-mishkili-elfu-sehemu-ya-kwanza

Maswali-na-mishkili-elfu-sehemu-ya-kwanza

Publication year :

2008

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Maswali-na-mishkili-elfu-sehemu-ya-kwanza

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la Alfu Suaal wa Ishkaal -sisi tumekiita Maswali na Mishkili Elfu kilichoandikwa na Shaikh Ali al-Kuraani al-Aamili na tumekigawa katika mijalada sita, na hili ulilonalo sasa ni jalada la kwanza. Madhehebu ya Shia Ithnaasharia imekuwa ikishutumiwa na Waislamu wengine shutuma ambazo hazina msingi wala hazimo katika imani na itikadi zake. Shutuma hizi zimekuwa zikirudiwa mara kwa mara licha ya kutolewa majibu madhubuti na yakinifu na wanavyuoni wa zamani na wa sasa. Kutokana na kasumba hii, mwandishi wa kitabu hiki ameamua kukusanya maswali na mishkili elfu moja kutoka kwenye vitabu vya Kisunni na kutoa hoja kabambe kuzijibu shutuma hizo wanazozuliwa wafuasi wa madhehebu ya Shia. Katika kulitekeleza jukumu hili, mwandishi ametegemea rejea zao za msingi kutoka katika (vitabu vya) hadithi, tafsiri, fikihi na itikadi, na kauli za viongozi wao wakubwa kuanzia wa zamani hadi wa sasa. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu. Katika wakati ambao maadui wa Uislamu na Waislamu wameamua kuungana ili kuubomoa Uislamu, na katika kutekeleza azma yao hii mbinu yao kubwa ni kutumia hitilafu zetu za kimadhehebu; hivyo, tunakitoa katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na yaliyomo katika safu hii ya masomo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya kidini na ya kijamii.