Mateso ya Dhuria ya Mtume

Mateso ya Dhuria ya Mtume

Mateso ya Dhuria ya Mtume

Interpreter :

Salman Shou

Publication year :

2013

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mateso ya Dhuria ya Mtume

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Sufferings of the Prophet’s Descendants, kilichoandikwa na Ustadh Murtadha Mutahhari. Sisi tumekiita, Mateso ya Dhuria ya Mtume. Ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha sana kuona kwamba historia ya Uislamu imejaa mateso waliyofanyiwa Dhuria ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), Mtume ambaye ni rehema kwa ulimwengu lakini kwa Kizazi chake imekuwa kwao ni mateso yasiyomithilika. Sababu ya kufanyiwa mateso hayo kunatokana na kutaka kwao kusimamisha haki katika ulimwengu kwa kufuata nyayo za Mtukufu Mtume. Makafiri walimfanyia Mtume (s.a.w.w) vitimbi vya kila aina, lakini hatimaye kwa uwezo wa Allah aliweza kuwashinda na Uislamu ukasimama na kuwa imara. Lakini baada tu ya kufariki Mtume (s.a.w.w) waliibuka watawala madhalimu ambao walipinga mafundisho ya Uislamu ya kuleta usawa na haki kwa watu wote. Hivyo, ili kutekeleza malengo yao ya kidhalimu, waliwatesa na kuwauwa Dhuria ya Mtume (s.a.w.w) au kwa jina lingine Ahlul Bayt (a.s) ambao ndio waliokuwa na dhamana ya kuhakikisha kwamba Uislamu unaendelea kusimama na kustawi. Kitabu hiki kimekusanya maelezo ya mateso ya Ahlul Bayt (a.s.) kutoka kwenye majilisi 61 (hotuba za maombolezo) za Ustadh Shahid Murtadha Mutahhari ambazo zinaweza kukidhi haja ya wasomaji wa majilisi kwa kiwango fulani. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu. Kutoka na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu Salman Shou kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Aidha tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin.