Maulidi si bida si haramu

Maulidi si bida si haramu

Maulidi si bida si haramu

Publication year :

2002

Publish location :

Mombasa Kenya

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Maulidi si bida si haramu

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa viumbe vyote. Na swala na salamu zimshukie
Hashimu, Mtume Wake muadhamu (s.a.w.w.), na aali zake kiramu, na wote wenye kufuata nyayo zao.
Baina ya tarehe 4 Rabiiul Awwal, 1423 / 17 Mei, 2002 na 7 Jamaadath Thaani, 1423 / 16 Agosti, 2002
nilitoa mfululizo wa makala kumi na tatu juu ya maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Katika makala
hayo, kwa kujibu hujja zinazotolewa na wale wanaopinga maulidi, nilijaribu kuonyesha kuwa maulidi si
bid'a (uzushi) wala si haramu.
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa makala hayo kupokewa vizuri na wote walioyasoma. Na
kwa kuitika maombi yao ya makala hayo kuchapishwa kitabu, nina furaha kubwa kuweza kuwatolea
kitabu hicho kama walivyotaka.
Makala hayo na kitabu hiki kisingetoka kama si kwa msaada wa ndugu kadhaa wa kadhaa waliojitolea
kunisaidia. Kwa upande wangu, sina la kuwalipa isipokuwa kuwaombea Mwenyezi Mungu awajazi kila
lenye kheri na wao; amin.