Mazungumzo-katika-dini-utamaduni-na-jamii
Mazungumzo-katika-dini-utamaduni-na-jamii
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2018
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Mazungumzo-katika-dini-utamaduni-na-jamii
Kitabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, Ahadith fi„d-Din wa „th-Thiqafah wa „l-Ijtima‟, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita kwa Kiswahili, Mazungumzo katika Dini, Utamaduni na Jamii. Kitabu hiki kimekusanya khutba na mihadhara iliyokuwa ikitolewa na Sheikh wetu huyu katika nyakati na sehemu mbalimbali Katika mfululizo wa vitabu vya mwandishi huyu, anahimiza waumini kuishi kwa kufuata mafundisho ya Uislamu ambayo yanagusa kila nyanja ya maisha na kiroho. Katika kitabu hiki anazungumzia juu ya mahusiano kuanzia katika familia, ndugu, jirani, jamii na utamaduni.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa
madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu Abdul Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili; pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera Amin.