Mfumo wa Wilaya

Mfumo wa Wilaya

Mfumo wa Wilaya

Interpreter :

Mohammad Said Kanju

Publication year :

2014

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mfumo wa Wilaya

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, The System of Wilaya. Sisi tumekiita, Mfumo wa Wilaya. Wilayah maana yake ni uongozi, usimamizi, utawala au uendeshaji wa jambo au kitu. Maana mojawapo kati ya istilahi hii, Kiislamu wilayah, ni mfumo wa uongozi baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na msingi wake ni kuanzia tukio la Karamu ya Ndugu (aqrabaa) mpaka tukio la Ghadir Khumm. Katika kitabu hiki, mwandishi anatuelezea kwa ufasaha kabisa kuhusu suala la wilayah kwa kuzingatia aya za Qur’ani na hadithi ambazo zinazungumzia suala hili na maana yake. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya kielimu ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itra imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.