Mizani ya hekima sehemu ya tatu

Mizani ya hekima sehemu ya tatu

Mizani ya hekima sehemu ya tatu

Interpreter :

Hemedi Lubumba

Publication year :

2018

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Mizani ya hekima sehemu ya tatu

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Mizanu‘l-Hikmah kilichoandikwa na Sheikh Muhammad Reyshahri. Sisi tumekiita, Mizani ya Hekima. Hiki ni kitabu cha utafiti juu ya hadithi zilizopokelewa moja kwa moja kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa Ahlul Bait (a.s.). Katika utafiti wake, mwandishi amerejea vitabu muhimu kabisa vya hadithi vilivyoandikwa na maulamaa wakubwa wa Kisunni na Kishia, k.v. Bukhari na Kulaini, n.k. Msingi wa kitabu hiki ni maneno ya mwenyewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliyotuachia au aliyotuusia juu ya Umma huu pale aliposema kwamba, “Nakuachieni vizito viwili - Kitabu cha Allah na Ahlul Bait wangu, na kwamba viwili hivi havitaachana mpaka vinifikie katika hodhi ya Kauthar.” Hivi ndivyo vitu alivyotuachia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na akasisitiza maneno yake haya kwa kusema: “Mtakaposhikamana na viwili hivi hamtapotea asilani…na mtakapoviacha viwili hivi au kimojawapo mtatengana na mtakuwa katika makundi ya Shetani.” Hapa mtu anaweza kujiuliza kwamba Kitabu cha Allah ni sawasawa. Lakini vipi Ahlul Bait? Jibu ni kwamba wao ni safi na Allah Mwenyewe Ndiye aliyewasafisha na kuwatakasa pale aliposema katika Sura ya al-Ahzaab, aya ya 33: “…..Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba (Ahlul Bait) ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”