Nani Mwenyezi Mungu?
Nani Mwenyezi Mungu?
Author :
Interpreter :
(0 Kura)
(0 Kura)
Nani Mwenyezi Mungu?
Wengi miongoni mwa watu, kwa kujidhani kuwa hawana wanayepaswa kuwajibika kwake katika maisha yao ya kila siku, wameshindwa kutafakari juu ya muujiza na maajabu ya ukubwa wa Ulimwengu wanaoishi. Lakini hata kama wangaliweza kufanya hivyo, wasingaliweza kuuzingatia ukubwa huo ingawa kutafakari kwao kungaliwafikisha kuukiri ukweli unaojidhihirisha katika umbile la Ulimwengu kuwa umeumbwa na Muumbaji Hodari, Fundi, Mwenye uwezo usiyomithilishwa, na Hekima iliyopindukia uwezo wa kufikiri alionao Mwanaadamu. Tuchukue upana wa mji mkubwa mmoja ambao watu wanaishi, tuuangalie kutoka upande mmoja hadi mwingine. Itatudhihirikia kuwa upana huu ni mkubwa mno. Labda tutumie njia nyingine katika kuelewa jambo hili. Tujaalie tumeweza kusafiri kutoka upande mmoja wa nchi yetu hadi mwingine, yaani kutoka mashariki hadi magharibi, hiyo piya haitaweza kutusaidia bali tutashangazwa tu na ukubwa wa eneo la nchi! Huu ni mfano mdogo wa kututia fikirani. Yawezekana wengi kama si wote, wameshasafiri kwa magari ya mabarabarani au ya relini kwenda sehemu za mbali ndani au nje ya nchi. Hebu zivutwe fikira juu ya suala moja muhimu, nalo ni hili. Hivi kuweza kusafiri kuzunguka sehemu zote za Dunia kwaweza kusaidia kuuhisi ukubwa wa Ulimwengu? Jawabu litakuwa hapana. Hiyo ni kwa sababu ukubwa wa Dunia unachukua nafasi iliyo sawa na vumbi kwa kulinganisha na ukubwa wa Ulimwengu huu ambao nao ni sehemu tu katika vile vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu. Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mbora wa kuumba!