PAMOJA NA MITUME KATIKA NJIA YA MASHAKA
PAMOJA NA MITUME KATIKA NJIA YA MASHAKA
Author :
Interpreter :
(0 Kura)
(0 Kura)
PAMOJA NA MITUME KATIKA NJIA YA MASHAKA
Mpenzi msomaji! Assalaamu alaykum wa rahmatullahi wa barakaatuh! Je, imetokea siku moja kuwa na shaka na ukahisi upweke katika njia ya haki kwa sababu ya uchache wa wafuasi wake? Je, umejikuta siku moja uko peke
yako katika uwanja wa mapambano? Je, umewahi kuzunguka huku na huko ukimtafuta mtu atakayekusaidia kutatua matatizo ya maisha na njia yake ngumu? Je, umewahi siku moja kuhitajia akiba ya chakula kwa ajili ya safari ya maisha ya mashaka? Je, yamekutokea yote hayo?
Sitangoja jibu kutoka kwako! Kwani jibu la watu wote litakuwa moja tu, nalo ni: "Ndiyo. Mambo hayo yote yametufika." Ndugu yangu Mwislamu! Hakika hukuwa peke yako katika njia iliyokupwekesha; wametangulia
katika njia hiyo Mitume watukufu, wanaharakati na wanamapinduzi wa mwanzoni. Hakika hukuwa peke yako katika uwanja wa mapambano uliosimama kuutetea Uislamu na itikadi za Waislamu, bali walitangulia mawalii na watu wema katika uwanja huohuo na mahali hapohapo ambapo ulisimama kwa lengo hilohilo na matumaini hayohayo uliyokuwa nayo.
Basi njia ni moja kufuatana na malengo na matumaini yake. Kwa hivyo, hukuwa peke yako. Pengine umekuwa peke yako katika wakati wako ambao ulifuata njia hiyo, lakini hukuwa peke yako katika nyakti zote ambazo amefaradhia Mwenyezi Mungu kukata mbuga ya maisha yenye miba.
Mitume watukufu, maimamu wema, wanaitikadi (wenye kubeba ujumbe) wa mwanzoni na mashahidi watukufu, kila mmoja wao ameingia katika majaribio hayo magumu ya kiitikadi, akayakabili na kuyavumilia kwa msimamo thabiti. kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamlipa malipo yake bila ya kupungua chochote. Basi makusudio yetu tunapokwenda katika njia yenye kudumu ya hao waliotutangulia ni kuwafuata na kuchukua mwanga wa taa yao na azma, subira na msimamo wao