Sura_al_Ahzaab_Tafsiri_na_Maelezo

Sura_al_Ahzaab_Tafsiri_na_Maelezo

Sura_al_Ahzaab_Tafsiri_na_Maelezo

Publication year :

2005

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Sura_al_Ahzaab_Tafsiri_na_Maelezo

Jina Sura hii imepata jina lake la Al-Ahzaab (makundi) kutoka aya ya 20 ya sura hii. Ilipoteremshwa Kama tunavyojua, Qur’ani Tukufu ina jumla ya sura 114. Sura hizo zimegawanywa mafungu mawili makubwa kwa kutegemea muda ambapo aya zake ziliteremshwa. Zile zilizoteremshwa wakati Bwana Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa bado yuko Makka (hajahamia Madina) huitwa Makkiyya (za Makka), na zile zilizoteremshwa baada ya kuhamia Madina huitwa Madaniyya (za Madina). Kwa kuwa inazungumzia matukio matatu muhimu katika historia ya Kiislamu, ambayo yote yalitokea baada ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) kuhamia Madina, sura hii huitwa Madaniyya. Matukio hayo ni yale ya Vita vya Handaki (au Makundi) vilivyokuwa katika Shawwaal (Mfungo Mosi) ya mwaka wa 5H; mashambulizi ya Banii Quraydhwa yaliyofanywa katika Dhil Qa’dah (Mfungo Pili) ya huohuo mwaka wa 5H; na ndoa ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) kumuowa Bi. Zaynab bt. Jahsh ambayo vilevile ilikuwa katika hiyo Dhil Qa’dah ya mwaka wa 5H. Yanayozungumzwa humu Ukizitaamali khalfia za sehemu kubwa ya aya zake, utaona kwamba sura hii haikushughulika na muktadha mmoja au maudhui mamoja, bali imeshughulika na maudhui mengi mbalimbali. Mwanzo kabisa (aya ya 1-3) Bwana Mtume (s.a.w.w.) na, kwa kupitia kwake yeye, Waislamu wote wanaamrishwa na kuonywa kwamba wasiwafuate makafiri na wanafiki katika ukafiri na unafiki wao, bali wafuate yale ya Mwenyezi Mungu peke yake na wamtegemee Yeye; wasitegemee nguvu zozote nyengine. Aya tatu hizo zimetangulizwa ili ziwe ni mwongozo wa kuamulia migongano iliyotokea baina ya Uislamu na ya Ukafiri yanayoelezwa katika aya zinazofuatia. Ili kuyafafanua hayo, aya mbili zinazofuatia (ya 4-5) zinatunabihisha mtu mmoja hawezi kuwa na nyoyo mbili katika kifua kimoja hata aweze kufuata mambo mawili yanayopingana. Haiwezekani kuyaamini yanayoamrishwa na Uislamu, na wakati huohuo ukayaamini yanayolekezwa na Ukafiri. Ukifanya hivyo, hutakuwa Mwislamu tena, bali utakuwa mnafiki moja kwa moja - sifa ambayo ni mbaya zaidi kuliko ile ya kuwa kafiri! Kwa msingi huo basi, ndipo Waislamu walipowekewa ile sharia ya kubatilisha dhihaar (tiz. Kidokezo Na. 4 humu) na ile ya kutowafanya watoto wao wa kupanga kuwa sawa na watoto wao khaalisa.