UislamU safi KatiKa maneno na UjUmbe wa imam Khomeini (r.a)

UislamU safi KatiKa maneno na UjUmbe wa imam Khomeini (r.a)

UislamU safi KatiKa maneno na UjUmbe wa imam Khomeini (r.a)

Publication year :

2011

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UislamU safi KatiKa maneno na UjUmbe wa imam Khomeini (r.a)

K itabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kifarsi kiitwacho, Islam-e-Naab dar Kalaam wa Payaame-Imam Khomeini (Pure Islam – Selected from the Speeches and Messages of Imam Khomeini) kilichochapishwa na Taasisi ya Majumui ya Uchapishaji wa Athari za Imam Khomeini (r.a.). Sisi tumekiita, Uislamu Safi. Kitabu hiki kinaelezea harakati za Imam Khomeini (r.a.) katika kuihudumia dini, na jinsi ambavyo aliipa uhai dini hii baada ya kukanyangwa na maadui wa Uislamu wa ndani na wa nje. Katika kitabu hiki, utaona mbinu alizotumia mwanachuoni mchamungu huyu mpaka kufanikisha Mapinduzi Makubwa ya Kiislamu, si nchini Iran tu bali ulimwenguni kote athari ya Mapinduzi haya imeenea. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo maadui wa Uislamu wameungana ili kuuangamiza. Lakini kama ailivyosema Allah (‘Azza wa Jalla) katika Qur’ani Tukufu: “Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru Yake ijapokuwa makafiri watachukia.” (9:32) Allah anasema kweli, kwa hakika hawatafani-
kiwa katika njama yao hii.
Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunaishukuru taasisi ya Hazrat Zahra Foundation of Tanzania kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.
Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni chenye manufaa na changamoto kubwa kwa wasomaji wetu.