UTAMADUNI WA MWAMKO WA KIJAMII

UTAMADUNI WA MWAMKO WA KIJAMII

UTAMADUNI WA MWAMKO WA KIJAMII

Publication year :

200

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UTAMADUNI WA MWAMKO WA KIJAMII

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya Kiswahili ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Thiqafatu ‘n-Nahdhi ‘l-Ijtima’iyyi, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii.
Utamaduni (thiqafah) maana: ni kukua na kukomaa kwa fikra na mwili wa mwanadamu kutokana na mafunzo na uzoefu wa kufanya kazi. Maana nyingine: ni hali ya maendeleo ya maarifa, elimu ya watu, ustaarabu, fani zote (za kielimu), imani, mila, desturi na asasi za kijamii zitambulishazo jamii. Kwa ujumla, hii ndio maana ya utamaduni kama ilivyofasiliwa katika Kamusi ya TUKI.
Uislamu ni mila na utamaduni ulioletwa na Mitume waliotumwa na Mwenyezi Mungu ili kuwafundisha wanadamu mila na utamaduni huu. Kama maana ya neno utamaduni inavyoonesha hapo juu, Uislamu umeletwa ili kuuboresha na kuukamilisha utamaduni huo. Mitume wote waliotumwa na Mwenyezi Mungu (takriban 124,000) kuanzia Mtume Adam mpaka Mtukufu Mtume Muhammad, kazi yao ilikuwa kufundisha utamaduni huu wa Kiislamu katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu - kimwili na kiroho. Ndio maana tunasema: “Uislamu ni mfumo kamili wa maisha.” Mwandishi wa kitabu hiki anaelezea kwa uzuri kabisa kuhusu utamaduni huu kwa kutaja vipengele muhimu kwa kurejea katika Qur’ani Tukufu, Sunnah, historia ya Kiislamu na matukio yake, n.k. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya kielimu ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetuAlhaji Abdul-Karim Juma Nkusuikwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Aidha, tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera  Amin.