UWAZI BAINA YA MASLAHI NA VIKWAZO

UWAZI BAINA YA MASLAHI NA VIKWAZO

UWAZI BAINA YA MASLAHI NA VIKWAZO

Publication year :

2014

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

UWAZI BAINA YA MASLAHI NA VIKWAZO

K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Infitah bayna ‘l-Masalih wa ‘l-Hawajis kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa al-Saffar. Sisi tumekiita, Uwazi baina ya Maslahi na Vikwazo.
Kitabu hiki kimetokana na semina zilizofanyika huko Awamiyah, Mkoa wa Qatif, Saudi Arabia.Lengo la semina hizo ni kuongeza maarifa na ujuzi wa waumini na pia kueneza moyo wa upendo licha ya kuwepo tofauti katika mitazamo ya kimadhehebu. Sisi wachapishaji tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo humo, wayafanyie kazi na kuyazingatia na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake.
Hivyo, ni matumaini yetu kwamba wasomaji wetu watanufai ka vya kutosha kutokana na kitabu hiki, kwani tumekiona ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia, matusi, kashifa na kugombanishwa wenyewe kwa
wenyewe ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Hii ni moja kati ya kazi kubwa zilizofanywa na Taasisi ya Al-It- rah katika kuwahudumia kielimu wasomaji wake wazungumzaji wa Kiswahili. Na kwa maana hiyohiyo, imeamua kukichapisha kitabu hiki chenye manufaa makubwa kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo lake lilelile la kuwahudumia Waislamu, hususan wanaozungumza Kiswahili.
Tunamshukuru mwandishi wa kitabu hiki, Sheikh Hasan Musa al-Saffar kwa kazi kubwa aliyofanya kwa ajili ya Umma huu wa Waislamu, Allah ‘Azza wa Jallah, amlipe kila la kheri na amuingize Peponi kwa salama na amani insha’Allah. Halikadhalika tunam shukuru Ndugu yetu Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukitarjumi kwa Kiswahili kitabu hiki, insha’Allah na yeye Allah Tabaraka wa Ta’ala, amlipe kila kheri hapa duniani na Akhera; pia bila kuwasa-
hau wale wote waliochangia kwa namna mmoja au nyingine mpaka kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na huko Akhera.