VIJANA NA MATARAJIO YA BAADAYE
VIJANA NA MATARAJIO YA BAADAYE
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2013
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
VIJANA NA MATARAJIO YA BAADAYE
Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, ash-Shabaab wa Tatallu’aat al-
Mustaqbal, kilichoandikwa na Sheikh Hassan Musa al-Saffar. Sisi tumekiita, Vijana na Matarajio ya Baadaye.
Uislamu ni dini na ni mfumo kamili wa maisha. Kwa maana hiyo Uislamu mbali na kuwaendeleza waumini wake kiroho, huangalia pia na maendeleo ya waumini wake kimaisha katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Uislamu pia huingia katika kila wakati na kufanya matakwa ya wakati husika kuafikiana na Uislamu bila kuathiri misingi yake. Hiki ndicho alichofanya mwandishi Sheikh wetu huyu anaangalia changamoto zinazowakabili vijana wa zama hii katika nyanja zote, kiroho na kimaisha na kushauri njia za kukabiliana nazo kwa mtazamo wa Kiislamu.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja
zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni vitu ambavyo havina nafasi tena katika akili za watu.
Kutoka na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tunamshukuru ndugu yetu Abdul-Karim Juma Nkusui kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitabu hiki
kwa Kiswahili kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au
nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera – Amin.