Wasifu Mfupi wa Imam Muhammad bin Hasan (a.s.)

Wasifu Mfupi wa Imam Muhammad bin Hasan (a.s.)

Wasifu Mfupi wa Imam Muhammad bin Hasan (a.s.)

Interpreter :

MUHAMMAD S. KANGU

Publication year :

2013

Publish location :

Dar es salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Wasifu Mfupi wa Imam Muhammad bin Hasan (a.s.)

Hivi ndivyo ilivyoanza. Nilipokea barua kutoka kwa Mhubiri Mkuu wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, Allama Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, akiniomba niandike masomo ya kufundisha kwa ajili ya Masomo ya Kimataifa kwa njia ya Posta juu ya Historia ya Uislamu ambayo Taasisi hii imekusudia kuyafanya. Kuwa muwazi zaidi, jukumu langu lilikuwa ni kuandika Vitengo (Units) tofauti 13, katika muundo wa vijitabu, vikiwa na maelezo mafupi ya wasifu wa maisha ya Hadhrat Fatima (s.a.) na Maimam Masoom 12. Madhumuni yalikuwa: Vijitabu hivi viwe rahisi kusomwa, vikikusudiwa kwa ajili ya Mashia/Waislamu wapya na vijana wa jumuiya ya Waislamu, wanaotafuta elimu kuhusu Maimam Masoom. Allama Rizvi kwa makhususi alisema kwamba vijitabu hivi havikukusudiwa kwa ajili ya wanachuoni bali wasomaji wa kawaida na kwa hivyo lazima viepuke mitego ya kiusomi. Kwangu mimi, ina maana ya heshima ya pekee na utambuzi. Kwamba Allama Rizvi, mmoja wa waandishi na mwanachuo mashuhuri katika ulimwengu wa Shia, lazima ameniona mimi kuwa na uwezo wa kuelewa majukumu haya, ni kitu ambacho kamwe sijawahi kukiwazia katika ndoto zangu za kawaida! Sasa kwa vile fursa hii ilikuwepo pale, nilikubali changamoto hii kwa sababu mbili. Kwanza, hii itanipa mimi fursa adimu ya kufanyakazi chini ya usimamizi wa karibu wa Allama Rizvi, ambaye mwongozo wake utafungua maeneo makubwa ya ujuzi kwa ajili yangu katika nyanja muhimu za Historia ya Uislamu. Pili, nitakuwa ninafanya kazi ambayo inaweza kuwa sababu kwangu mimi kupata ‘SAWAB-E- JARI’ mara tu nitakapoondoka ulimwenuni hapa kwenda Akhera.