HAJA YA DINI

HAJA YA DINI

HAJA YA DINI

Publication year :

1999

Publish number :

Toleo ya Tano

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

HAJA YA DINI

Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu chake kiitwacho Need of Religion alichokiandika kwa lugha ya Kiingereza, kwa ajili ya vijana wa Kiislamu wanaochukua Stashaada (Diploma) ya Elimu ya Kiislamu kwa Njia ya Posta. Nimeona kuwa kitabu hiki kitawasaidia sana ndugu zangu Waislamu wa hapa Afrika ya Mashariki, iwapo nitakitarajumu kwa Lugha ya Kiswahili, lugha ambayo hutumiwa sana hapa kwetu. Kila mtu hupenda kitu na kukithamini sana baada ya kukiona kuwa ni cha faida kake. Kadiri ya faida ya kitu hicho itakavyozidi ndio jinsi mtu huyo atakavyozidi kukithamini na kukipenda kitu hicho. Dini nayo ni hivyo hivyo. Mtu ataipenda tu, baada ya kuzielewa faida zake kwake. Katika kijitabu hiki, ndugu yetu Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, kwanza anaeleza Dini ni nini, kisha anaelezea faida zake, anakanusha hoja za wale wasemao kuwa dini ni kitu kipingacho sayansi n.k. Analinganisha dini na “Maendeleo na Mabadiliko ya viumbe”, halafu anakanusha hoja za wale wasioamini kuwepo kwa siku ya Ufufuo. Mwisho kabisa anamalizia kwa kuzitaja sifa muhimu za dini. Sifa zote ni zake Mwenyezi Mungu aliyemjaalia ndugu yetu Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi kwa elimu na akatunufaisha sisi Waislamu wa hapa Afrika Mashariki na duniani pote kwayo.