Hotuba-za-Kiislamu-juu-ya-haki-za-Binadamu

Hotuba-za-Kiislamu-juu-ya-haki-za-Binadamu

Hotuba-za-Kiislamu-juu-ya-haki-za-Binadamu

Interpreter :

Muhammad A. Bahsan

Publication year :

2015

Publish location :

Tanzania Dar es salaam

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Hotuba-za-Kiislamu-juu-ya-haki-za-Binadamu

Kitabu ulichonacho mikononi mwako ni kitabu ambacho asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la: al-Khitwabul-IslamiyWahuququl-Insan Kilichoandikwa na Sheikh Hassan Musa al-Saffar. Na sisi tumekiita: “Haki za Binadamu” kwa Kiswahili Haki za binadamu ni suala ambalo limepigiwa kelele sana na wapenda haki na amani duniani, na hii imetokana na haki hii kuvunjwa kwa makusudi na watu madhalimu na na tawala kandamizi duniani. Aidha, Uislamu ni wa kwanza katika kuainisha haki hizo za binadamu na kuzisimamia kikamilifu. Hapa lazima ieleweke kwamba nazungumzia Uislamu na sio Waislamu, kwa sababu kuna baadhi ya Waislamu na serikali zinazojiita za Kiislamu ambazo ziko juu katika kuvunja haki za binadamu. Uislamu uko mbali na watu hao na serikali hizo. Hivyo msimamo na mafunzo ya Uislamu huhakikisha kwamba haki za binadamu zinalindwa na kutekelezwa kama ilivyo. Na humkemea na kumlaumu kila mwenye kuzivunja haki hizo bila kujali kama yeye ni Mwislamu au la. Mwandishi wa kitabu hiki anatumia kalamu yake kuelezea utukufu wa binadamu na maisha yake na jinsi ya kusimamia haki zake za msingi na kuzitekeleza Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo ulimwengu umejaa dhulma na uonevu unaofanyiwa ubinadamu.