KUTOFAUTIANA NA KUISHI KWA PAMOJA

KUTOFAUTIANA NA KUISHI KWA PAMOJA

KUTOFAUTIANA NA KUISHI KWA PAMOJA

Interpreter :

Sheikh Shafi Nina

Publication year :

2000

Publish location :

Dar es Salaam Tanzania

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

KUTOFAUTIANA NA KUISHI KWA PAMOJA

K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, at-Tanawwu’ wa at-Ta’ayish, kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Safar. Sisi tumekiita kwa Kiswahili, Kutofautiana na Kuishi Pamoja.
Kutofautiana ni hulka ya wanadamu, hivyo, watu hutofautiana katika mambo mengi, k.v. katika utamaduni, itikadi za kisiasa na za kidini, n. k. Lakini watu wanaishi pamoja na kuvumiliana, na haya ndio maudhui ya kitabu hiki.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo kuna mifarakano mingi inayosababishwa kwa makusudi na watu waovu ulimwenguni ili kukidhi haja na maslahi yao maovu.
Kutokana na ukweli huu, taasisi yetu ya Al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumini yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.   Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Shafi Nina kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kukitarjumi kitbu hiki kutoka lugha ya asili ya Kiarabu. Pia na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Allah awalipe wote malipo mema hapa duniani na kesho Akhera  Amin