MADHEHEBU ZA KISHIA

MADHEHEBU ZA KISHIA
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2004
Number of volumes :
1500
Publish number :
Chapa ya Kumi
Publish location :
Dar es Salaam, Tanzania
(0 Kura)

(0 Kura)
MADHEHEBU ZA KISHIA
Tunamshukuru Allah (s.w.t.), kwa Baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Watukufu Ahlul~Bait (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha Toleo hili la kumi la kitabu hiki “Madhehebu Za Kishia”.
Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya moja ya maandishi ya Allamah al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi (r.a.). Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Ki-Islamu na kilitafsiriwa na kuchapishwa na Taasisi mbali mbali kwa lugha ya Ki-Ingereza na Ki-Urdu.
Tafsiri hii ya Kiswahili ilichapishwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1985 na sasa mwaka wa 2004 kinachapishwa toleo hili la kumi na kufikia nakala elfu kumi na nne, hii inaonesha kwamba kitabu hiki kinapendwa na kupata umarufu na watu kote Afrika ya Mashariki.
Bilal Muslim Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa mfasiri wa kitabu hiki Ndugu Maalim Dhikiri U. M. Kiondo na wale wote ambao kwa juhudi zao kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi mwao na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine katika kazi zetu za Tabligh, Tunamuomba Allah (s.w.t.)
awalipe malipo mema hapa Duniani na baadaye huko, Akhera.






