Mafunzo ya Awali ya Uislamu
Mafunzo ya Awali ya Uislamu
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2000
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
(0 Kura)
(0 Kura)
Mafunzo ya Awali ya Uislamu
Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho “Elements of Islamic Studies” kilichoandikwa na Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi Toleo la Kiingereza la kitabu hiki “Elements of Islamic Studies” lilitolewa mnamo tarehe 15 ya mwezi wa Shaaban, 1388 A.H. (7/11/1968) na Haji Mohamed A. Khimji. Kitabu hicho kilitumika katika mafunzo ya Dini katika shule za Sekondari. Katika muda mfupi tu, kitabu hicho kilimalizika, lakini kuhitajika kwake kuliongezeka kila siku. Hivyo, Misheni yetu ikaamua kukichapisha tena. Toleo hilo lilisahihishwa kabisa-kabisa (kwa mujibu wa Fatwa ya Agha Sayyid Abul Qassim al-Khui, Dama Dhulluhul-Aali, Najaf, Iraq). Pia Mafunzo mengi mengineyo yameongezewa kwa sababu ya kuhitajika kwake kwingi kwa mfano, maelezo ya ghusli kwa kirefu, Sala za Ayat, Ijumaa, Iddi Mbili, Mayyit na Jamaat. Tulipokiona kuwa ni chenye kuleta manufaa zaidi mashuleni tuliamua kukitafsiri kwa lugha ya kiswahili ili kiweze kutumika kama kitabu cha kufudishia hata katika shule za msingi. Twategemea kuwa kitabu hiki kitasaidia sana mashuleni mwetu katika kujenga msingi wa Dini ya Kiislamu miongoni mwa vijana wetu Insha Allahu Taala.