MWANAMKE KATIKA MAGEUZI
MWANAMKE KATIKA MAGEUZI
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2000
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
MWANAMKE KATIKA MAGEUZI
K itabu ulichonacho mikononi mwako asili yake ni cha lugha ya Kiarabu kwa jina la, al-Mar’ah wa ath-Tawrah kilichoandikwa na Sheikh Hasan Musa as-Saffar. Sisi tumekiita, Mwanamke na Harakati za Mageuzi.
Hiki ni kitabu kinachoelezea uwezo wa mwanamke katika mapambano ya kujikomboa kutoka kwenye makucha ya wakandamizaji na madikteta. Mwandishi wa kitabu hiki anatuletea visa ambavyo mwanamke alishiriki katika mapambano sambamba na wanaume na kuonesha ushujaa mkubwa sana kinyume na wanavyodhania watu wengine.
Uislamu haumbagui mwanamke katika kuhudumia jamii katika nyanja zote ilimradi tu awe katika mipaka ya sheria za Kiislamu.
Halikadhalika mwanamke katika Uislamu amepewa hadhi ya juu sana kuliko hata ya mwanamume. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu ambapo mwanamke anadhalilishwa sana bila ya yeye mwenyewe kujua. Wanatembezwa uchi, wamegeuzwa kuwa bidhaa huku wenyewe wakiwa wameridhika na kusema kwamba hiyo ndiohaki na usawa.
Taasisi yetu ya al-Itrah imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa na manufaa makubwa kwao.
pia. Amin!