Tafsiri ya Qur'ani Al-Miizanan

Tafsiri ya Qur'ani Al-Miizanan

Tafsiri ya Qur'ani Al-Miizanan

(0 Kura)

QRCode

(0 Kura)

Tafsiri ya Qur'ani Al-Miizanan

Katika kazi nyingine alizozifanya mfasiri mkubwa allama tabatabai Al-Mizan inachukuwa nafasi ya kwanza katika kutambuliwa, kwa sababu ya sifa zake zisizokuwa na kifani. Jambo hili si katika vitabu vyake tu bali ni katika vitabu
vyote vya Kiislamu vilivyo andikwa kuhusu Dini, Sayansi, Falsafa, na hasa kuhusu aina zote za tafsiri ya Qur'an mpya ama zamani zilizoandikwa na Sunni ama Shia. Maelezo haya hayawezi kueleza kwa urefu mambo yaliyomo lakini yanaweza kuwasaidia wasomaji kwa kuwapa fununu juu ya umaridadi wa Al Mizan. Ninaona kwamba sistahili kuifanya kazi kubwa kama hii kama watu wakubwa mfano Ayatullah Mutahhari ambaye yeye mwenyewe ni mtu
mwenye fikra mpya, mjuzi wa Qur'an na mfasiri vile vile, aliposema: "Al-Mizan ni tafsiri kubwa zaidi ya Qur'an iliyowahi kuandikwa tangu kuanza Uislamu; na itachukua miaka sitini ama mia moja mpaka watu wetu
kuutambua umuhimu wa Al-Mizan ya Allama Tabatabai. "Wanachuoni wengine, wajuzi na watu walio na busara walitoa maoni kama haya kuhusu kitabu hiki. Majaribio yoyote ya kuonyesha maana ndani ya Al- Mizan hata
kama ni kwa njia ya juujuu, katika maelezo mafupi kama haya, ni kama kujaribu kuitia bahari ya Atlantiki katika chungu kidogo.

Hata hivyo ninatarajia kukusanya matone machache katika bahari hii ya elimu ya Kiislamu kulingana na uwezo wangu ili nitosheleze kiu yangu. Nataraji roho njema ya mwandishi mcha Mungu wa kitabu hiki cha milele, itaniwia
radhi kwa kazi hii ndogo nitakayoitanguliza