Vipi TuTaishinda hofu?
Vipi TuTaishinda hofu?
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publication year :
2014
Publish location :
Dar es Salaam Tanzania
(0 Kura)
(0 Kura)
Vipi TuTaishinda hofu?
K itabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Kayfa Nuqhiru ‘l-Khawf kilichoandikwa na Sheikh Hasan as-Saffar. Sisi tumekiita, Vipi Tutaishinda Hofu?
Uislamu ni dini na mfumo kamili wa maisha; ni dini kwa maana ya kuihudumia roho ili kufikia kiwango cha juu cha uchamungu (takwa) kitu ambacho ndio lengo kubwa la muumini. Ili kufikia lengo hili, muumini huyu huongozwa na Qur’ani Tukufu ambacho ni Kitabu kisicho na shaka na ni mwongozo kwa wanadamu wote. Allah anasema: “Hicho ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake na ni mwonngozo kwa wamchao (Mungu).” (2:2) na:” Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo Qur’ani, kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi...” (2:185) Ni mfumo wa maisha kwa maana huhudumia maisha ya mtu hapa duniani, kwa ajili hiyo haikuacha kitu katika kumuongoza mwanadamu katika maisha yake ili aweze kuishi maisha mazuri na yenye kumpendeza Allah .
Kitabu hiki kinaelezea hofu. Wote tunajua kuna hofu nyingi ambazo huwafika watu na kuwafanya wasiishi kwa amani. Na hofu ziko aina nyingi, nyingine ni za kisaikolojia tu ambazo huwa na athari mbaya kwa mtu, hofu nyingine ni za kuogopa tu baadhi ya vitu au wanyama wakali, na nyingine ni hofu ya kumuogopa Allah
Mwandishi wa kitabu hiki amefanya juhudi kubwa ya kuelezea hofu hizi na jinsi ya kujinasua nazo au kuleta ufumbuzi wake kwa kurejea katika Qur’ani Tukufu na Sunna. Hakika msomaji atafarijika sana na yaliyomo katika kitabu hiki. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote.
Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.